Kufanikiwa kuna hatua ambazo wafanyabiashara na makampuni hupitia, ntaelezea baadhi ya hatua ili kuweza kukupa mafanikio katika biashara yako

Hatua

aid123138-900px-achieve-long%e2%80%90term-goals-step-151. Gundua vitu unavyotamani kuwa navyo. Inatakiwa uwe na mawazo ya maisha ya mbele . Andaa ndoto yako unayohitaji kuikamilisha na uwe tayari kuikamilisha.

aid123138-900px-set-smart-goals-step-162. Weka malengo katika biashara yako kwa kutengeneza plani ya biashara yako. Angalia unataka kufikia malengo gani ili uweze kujua ufanye nini na ni kwa mda gani.

aid123138-900px-fix-your-mistakes-step-2-version-23. Jifunze kutokana na makosa. ukijifunza kutokana na makosa utaweza kujua jinsi ya kuepuka makosa na kuto yarudia tena, jaribu kufanya mambo yenye manufaa.

aid123138-900px-be-a-hard-worker-step-74. Iheshimu na kuithamini biashara yako. Ukiwa na biashara yako unakuwa na uhuru, ila uhuru huo usikufanye ukatumia mda mwingi nje ya kazi/biashara. Biashara yako itadumu na itakuwa endapo utaiheshimu na kuithamini.

aid1256160-900px-enhance-personal-creativity-step-7
5. Kuwa mbunifu. Tafuta kitu kitakacho kutofautisha na wengine katika biashara
aid123138-900px-improve-service-quality-at-your-business-step-17-version-2
6. Kuwa tayari kusikiliza na kujibu maswali kutoka kwa wateja. Mteja ni mtu wa muhimu sana katika biashara, ili uweze kumfanya awe mteja wako wa kila siku na akuletee wateja wengine inatakiwa umsikilize kwa makini na kumjibu maswali yake.
aid123138-900px-write-a-financial-report-step-2-version-2
7. Tambua kuwa kila biashara inakuwa na hatari yake kwa kuingia hasara. usikate tamaa pale utakapo pata hasara kwani ni moja ya changamoto za kibiashara cha muhimu ni kuangalia makosa na kuyarekebisha.
aid123138-900px-improve-service-quality-at-your-business-step-24-version-2
8. Kuwa rahisi tangaza biashara yako. jaribu kuifanya biashara yako ifahamike na watu mbalimbali ili kutanua uwazi wa wateja kutoka sehemu mbalimbali kwa kuwapa taarifa juu ya bidhaa zako na huduma zako.
Advertisements